Jumanne , 24th Aug , 2021

Kenyan OG, Khaligraph Jones na Blaq Bonez rapper kutoka Nigeria wamaliza tofauti zao ambazo zilitokea mwaka 2020 baada ya OG kushinda tuzo ya MVP huko Nigeria.

Picha ya pamoja Msanii Khaligraph Jones na Blaq Bonez

Uadui wao wameumaliza kwa kuonekana studio pamoja wakihisiwa kupika pini jipya huku  Bien Sol wa Sauti Sol akiwa kama mwamuzi wa pambano lao ambapo kitendo hicho kimetafsiriwa kama ni ukomavu wa tasnia ya hip hop Afrika .

Blaq Bonez kwa sasa yupo nchini Kenya kwa siku kadhaa sasa akitangaza albamu yake ya mpya ‘Sex Over Love’ iliyotoka Aprili 30, 2021 chini ya Chocolate City.