Ijumaa , 4th Jul , 2014

Msanii maarufu wa kike raia Sweden mjini Stockholm mwenye makazi yake nchini Tanzania, Saraha amerudi nchini kwa ajili ya maandalizi ya kurekodi nyimbo na kushoot videos zake mpya.

Msanii wa bongo fleva Saraha

Saraha ameongea na eNewz kuwa anatarajia kuchukua muda usiopungua mwezi mmoja na nusu kufanya kazi hizo nchini, ambapo ameweka wazi kuwa wiki ijayo atatoa wimbo wake mpya alioubatiza jina 'Shemeji' ambao umetengenezwa nchini Sweden na prodyuza anayeitwa Memo Crecendo.

Mwanadada huyo ameongezea kuwa wakati wimbo huo ukiwa hewani anafanya maandalizi pia ya "kushoot" video ya wimbo huo nchini Tanzania chini ya kampuni ya Dream Production na kuongozwa na Raymond Kasoga.

Aidha, Saraha aliyepotea kwa kipindi kirefu nje ya nchi amesema kuwa atarudi tena nchini Sweden kumalizia masomo yake huku nyimbo zake nyingi zikipigwa katika vituo mbalimbali nchini humo ukiwemo wa 'Mbele Kiza' ulioingia Top Ten.