Jumatano , 4th Jun , 2014

Kili Music Tour 2014, inaendelea Kuzungusha Kikwetu kwetu, ambapo sasa kikosi kizima kimejipanga kwa ajili ya kuangusha bonge la shoo za aina yake Jumamosi hii ya tarehe 07, katika uwanja wa Halmashauri wa Kahama.

Kili Music Tour 2014 Kahama

Kikosi kazi kitakacho-tingisha jukwaa live bila chenga, kinahusisha wasanii wakali kabisa wanaosumbua katika chati za muziki hapa Bongo, akiwepo mwanadada Shilole, Christian Bella, Madee, MwanaFA, AY, Rich Mavocal, Jambo Squad pamoja na Weusi.

Itakuwa ni bonge moja la shoo, pale Kahama katika uwanja wa Halmashauri kuanzia saa 10 jioni, kwa kiingilio cha shilingi 2,500 tu na kama hiyo haitoshi utapata zawadi ya bia moja ya Kilimanjaro Buree.

Kili Music Tour 2014, Zungusha Kikwetu kwetu.