Jumanne , 20th Jul , 2021

Msanii wa Konde Gang Music Worldwide Killy ameisifia ngoma mpya ya 'Salute' ya boss wake wa zamani Alikiba ambayo ameifanya na Paul wa P Square 'King Rudy' kutoka nchini Nigeria.

Msanii Killy kushoto na Alikiba kulia

Killy anasema amependa ubunifu uliofanyika kwenye video ya wimbo huo na Alikiba amevaa uhusika na watu wamependa kilichofanyika.

"Nimependa creativity ya video Director ametisha sana na wimbo mkali, nimemuona kaka yangu Alikiba ame-act ile character ya kuuvaa uhusika kabisa, kitu ambacho kimefanyika ni kizuri na hata watu wamekipokea pia" amesema Killy

Ikumbukwe Killy na Cheed wote walikuwa chini ya Alikiba kwenye lebo ya Kings Music Records kabla ya kuhama April 2020, kuhamia lebo ya Konde Gang Worldwide ya Harmonize.

Zaidi tazama hapa chini kwenye video.