Kinachomfanya Bella akate simu ya shabiki

Ijumaa , 12th Jul , 2019

Mwimbaji Christian Bella, amefunguka kuwa simu kwenye maisha yake ni kitu cha muhimu sana na haijalishi inatoka kwa mtu anayemjua au asiyemjua, cha muhimu ni yeye kujua ina ujumbe gani.

Christian Bella

Kupitia DADAZ ya East Africa Television Bella amesema anapokea simu zote zinazoingia labda asiwe tu na muda au yupo studio anarekodi.

''Huwezi kujua ni simu ya aina gani inapigwa, inaweza kuwa ndugu yako anaumwa au mtu anataka kukuepusha na janga fulani, ila inakata sana pale shabiki anapokupigia tu analeta stori nyingi au kukuomba uongee na watu wake na wewe huna muda unalazimika kukata'', amesema.

Bella pia ameeleza kuwa moja ya starehe zake kubwa ni kucheza 'Play Station' anapokuwa nyumbani peke yake hususani kwasasa ambapo familia yake ipo Ulaya.

''Starehe yangu kubwa ni 'Play Station' yaani huwa nashinda nacheza nikiwa nyumbani. Starehe yangu nyingine ni kuwa studio, yaani nikiwa pale hata kama mwingine anarekodi mimi napata mzuka wa kuandika au kufanya chochote'' - Christian Bella.