Kingwendu arudisha fomu, ataja Jimbo analolichukua

Jumatatu , 6th Jul , 2020

Mchekeshaji wa muda mrefu Bongo Kingwendu amesema leo Julai 6, 2020 anarudisha fomu ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Ilala na ametaja vipaumbele vyake kama Maji, Shule na Hosptali.

Mchekeshaji Kingwendu

Kingwendu amesema tayari ameshapata wadhamini na hataweza kufilisika kwa kuuza nyumba na gari mbili kama ilivyomtokea kwenye kampeni za mwaka 2015, na amewaasa wasanii wengine wanaogombea Ubunge kuwa wasiwe lele mama kwenye siasa.

"Chama changu ni CUF na Matarijio yangu mambo yatakuwa safi na nimejipanga tofauti na mwaka 2015, Nilikuwa nataka niende tena Kisarawe ila ma-boss zangu wakanishauri na kuniomba nigombee Jimbo la Ilala, vipaumbele vyangu ni kuangalia shida za wananchi kama vile Maji, kuongeza Hospitali kila kata, shule na usafi" amesema Kingwendu 

Aidha Kingwendu ameongeza kusema kipindi cha kampeni za mwaka 2015 alikuwa peke yake ila sasa hivi amepata wadhamini hivyo hataweza tena kuuza gari au nyumba ili kuendesha shughuli zote za kampeni