Jumanne , 13th Sep , 2016

Jaji wa shindano la Dance100% Super Nyamwela amesema kutokana na kiwango ambacho kimeoneshwa na washiriki wa shindano hilo tangu lianze ni dhahiri kwamba upinzani kwenye fainali utakuwa mkubwa sana.

Jaji wa Dance100% Super Namwela

Akizungumza na EATV Nyamwela amesema kuna vipaji vingi sana ambavyo vipo kwa vijana ambao wameshiriki Dance100 jambo ambalo linaonesha wazi kwamba wakipata sapoti wanaweza kufika mbali zaidi.

“Ukiangalia walioweza kupenya hadi hatua ya nusu fainali, wameonesha kwamba ni wasanii ambao wanafaa kushiriki shughuli mbalimbali za kijamii ndiyo maana hata kwenye kutoa alama tunakuwa makini sana ili kuweza kuangalia kundi linaloonesha ubunifu zaidi la lingine” Amesema Nyamwela.

Aidha Nyamwela ameongeza kuwa makundi ambayo yamebahatika kutinga fainali yanajipanga kikamilifu kwa ajili ya kushiriki hatua ya fainali ambapo kundi litakaloshinda litapatikana kutokana na namna watakavyoonesha uwezo na ubunifu siku hiyo.

Shindano la Dance100% linadhaminiwa na Vodacom na Coca Cola na kuonyeshwa na EATV pekee kila Jumapili saa moja jioni.

Tags: