"Kuwa Bwege sio tatizo" - Selemani Bungara Bwege

Alhamisi , 6th Mei , 2021

Mzee wa 'Wewe ulisikia wapi' na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kilwa Seleman Bungara maarufu kama Bwege amesema kuitwa jina la bwege sio tatizo kwaki, ila tatizo linakuja je wewe ni bwege kweli au la.

Aliyekuwa Mbunge wa Kilwa Seleman Bungara 'Bwege'

Mbunge Bwege amesema jina hilo amelipata kwa Sheikh mmoja aliyekuwa akiishi maeneo ya Temeke Dar es Salaam ambaye ndio alikuwa anajiita jina hilo lakini aliongea vizuri na watu na hata yeye ana tabia hiyohiyo.

"Nilipata jina la bwege kutoka kwa Shekh mmoja pale Temeke aliyekuwa akiitwa Bwege lakini akawa ni Shekh mkubwa sana, alikuwa anajiita bwege, anakaa na kila mtu na anaongea na kila mtu na hata mimi ndivyo nilivyo, kwa hiyo bwege ni mtu ambaye yuko poa hapendi matatizo, unajua ubwege sio tatizo ila tatizo je wewe bwege kweli" ameeleza Seleman Bungara Bwege