Ijumaa , 24th Apr , 2015

Msanii na mtayarishaji mahiri wa muziki Lucci, amesema kuwa kati ya video za muziki za Hip Hop ambazo hazikubali, ni video ya Bongo Hip Hop ya staa wa muziki Fid Q aliyofanywa na rafiki yake wa karibu Nisher kutokana na kuwekwa filterz nyingi.

msanii na mtayarisha wa muziki nchini Lucci

Lucci ambaye ni mdau mkubwa wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini, ameeleza hayo kama sehemu ya maoni yake akiwa anaorodhesha video kali za Hip Hop anazozikubali zaidi katika mahojiano tuliyofanya naye hivi karibuni.