Lulu Diva adai ana miaka 19

Jumatano , 4th Sep , 2019

Msanii wa Muziki wa BongoFleva, Lulu Diva amesema yeye kwa sasa ana miaka 19 na atahakikisha anaingia kwenye ndoa pindi atakapofikisha miaka 25.

Lulu Diva ametoa kauli hiyo wakati akizungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, kinachorushwa kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8:30 mchana.

Lulu Diva amesema, "'kwasasa nina miaka 19, natarajia kuolewa nikifikisha miaka 25".

Aidha Lulu Diva amesema kuwa, "siwezi kuolewa na Barnaba ni ndugu yangu na baadhi ya mafaili yake nayajua, ila mimi ndio sina mafaili maana nimeingia saivi tu kwenye mahusiano".

Kwa sasa msanii huyo anatamba kwa ngoma ya Chekecha ambayo anatarajia kutoa video hivi karibuni.

Tazama mahojiano kamili hapo chini