Alhamisi , 20th Feb , 2014

Urembo waasili na mvuto alionao muigizaji filamu anayechipukia raia wa Kenya Lupita Nyong'o umezidi kuchochea umaarufu wake na safari hii nyota huyo amepamba jarida la DuJour.

Lupita ambaye ameteuliwa kuwania tuzo ya Oscar kwa uhusika wake kwenye filamu ya 12 Years A Slave, amepiga picha mbalimbali katika mapozi yenye mvuto kwenye jarida hilo.

Lupita Nyong'o ambaye alizaliwa Mexico, licha ya kuwa na kipaji cha kuigiza pia anatajwa kuwa ni binti mrembo anayekwenda sawa na mitindo.