"Mahari inaanzia buku, hatupandi" - Idris Sultan

Ijumaa , 15th Mei , 2020

Mchekeshaji maarufu hapa nchini Idris Sultan, ametangaza kiasi cha mahari ambacho ndicho atakachomuozesha dada yake Lulu Diva, na kusema kuwa mahari hiyo itaanzia Tsh 1,000.

Mchekeshaji Idris Sultan

Idris Sultan ameeleza hivyo kupita post yake aliyoweka katika mtandao wa kijamii wa Instagram ambayo inasema.

"Familia ya Sultan inatoa wito kwa yeyote atakayeweza kuwatua mzigo huu, muda unakwenda na familia ipo tayari kukaa chini kufanya majadiliano, mahari inaanzia buku na hatupandi zaidi ya hapo" amendika Idris Sultan.

Baada ya muda mfupi Lulu Diva mwenyewa akajibu kwa  "Hivi ndio mmefikia huku, mmeniweka kwenye mnada, Idris Sultan ila ujue huwez kuwa serious".