"Mahari yangu sio chini ya Milioni 20"- Agness

Jumanne , 2nd Mar , 2021

Mrembo Official Agness maarufu kama Agness wa Uchebe amefunguka kusema wanaume wanaotaka kumuoa mahari yake ni kuanzia shilingi Milioni 20 kama hauna hautaweza kumpata.

Mrembo Official Agness

Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital Agness wa Uchebe amesema sababu ya kutaja mahari hiyo ni kutokana alivyojitengeneza kwenye maisha yake, anavyojieweza na anavyojielewa.

"Mahari yangu mimi ni kubwa sana kwa sababu nimeshajitengeneza kwenye maisha yangu na najielewa, kama nyumba na gari vyote ninavyo pia nina biashara zangu kwa hiyo mahari  lazima iwe kubwa, mahari yangu sio chini ya Milioni 20 wanaume wajipange sana" amesema Agness wa Uchebe 

Zaidi mtazame hapa akilizungumzia hilo.