Jumatatu , 10th Aug , 2015

Majaji wa mashindano ya Dance 100%, wametoa tathmini yao baada ya kumalizika kwa usahili wa michuano hiyo kwa kishindo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam.

majaji wa mashindano ya kucheza muziki ya Dance 100% Super Nyamwela, Shetta na Queen Darleen

Katika michauno hiyo ya kusisimua kila mmoja kwa nafasi yake amefurahishwa na uwezo na vipaji vilivyopatikana kuelekea hatua ya robo fainali.

Super Nyamwela, Queen Darleen na Shetta kwa kifupi wameeleza namna kazi ilivyokuwa kubwa ikiibua vipaji vya kutosha licha ya changamoto za hapa na pale za makundi mwengine kutokujituma sana , kuweka mwembwe zaidi ya dansi na kujitokeza kwa wingi dakika za mwisho.

Kwa kuwasikiliza kwa kirefu majaji wakitoa tathmini yao, usikose kutazama kipindi cha Dance 100%, jumamosi hii, saa 12:30 jioni hapa EATV pekee.