Jumanne , 28th Apr , 2015

Kichupa ambacho kilikuwa kinasubiriwa kwa hamu sana na mashabiki cha wasanii wakali wa miondoko ya bongofleva mwanadada Saraha na Makamua kimeachiwa leo rasmi kupitia EATV.

wasanii wa bongofleva nchini Saraha na Makamua

Video ya wimbo huo mpya uliobatizwa jina 'Tuongee' ni wimbo ambao Makamua aliamua kumpa shavu diva huyo kwa jinsi alivyo mahiri katika kuchanganya lugha ya kiswahili na kiswedish na kuleta ladha tofauti katika muziki.

Saraha anatarajia kuufanyia uzinduzi rasmi wa wimbo huo nchini Tanzania huku akiendelea kupata sapoti mbalimbali za mashabiki wake nchini Sweden katika matamasha yake ya muziki ambapo ndio makazi yake kwa sasa.