Jumatatu , 22nd Aug , 2016

Baadhi ya makundi yanayoshiriki shindano la Dance100% yameanza kutambiana kila moja likisema ndilo litaibuka na ushindi na kujinyakulia kitita cha milioni 7 ambazo ndizo zitatolewa kwa mshindi mwaka huu.

Moja kati ya makundi yanayoshiriki katika shindano hilo

Wakizungumza na EATV kwa nyakati tofauti kundi la The Quest Crew wamesema mazoezi wanayoendelea nayo ni ya nguvu na ufundi wa hali ya juu ambapo wanaamini wataibuka na ushindi.

Mwenyekiti wa kundi hilo Brown Bryton amesema wao wanaamini kwamba ubunifu na kufuata maelekezo ya majaji lazima vitawafanya wanyakue ushindi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kundi la Tatanisha kutoka Mabibo amesema kundi lake limeshabaini udhaifu wa wenzao na ndiyo wanaufanyia kazi na imani yao ni kwamba wao ndiyo watachukua ushindi mwaka huu.

Aidha Mwenyekiti wa kundi la Ikulu Vegaz Ramadhani amesema kundi lake ni mara ya tatu kushiriki na nia yao siyo kushiriki kama miaka mingine ila mwaka huu wamepania kuchukua ushindi kwa kuwa makosa waliyorekebishwa na majaji wameyafanyia kazi na wanajiamini kwamba wao ndiyo watatangazwa washindi.

Makundi 10 ambayo yalifuzu hatua ya robo fainali yatashiriki hatua ya nusu fainali wili ijayo ambapo makundi matano yatabakia katika hatua ya fainali.

Shindano la Dance100% linaoneshwa na EATV siku ya Jumapili saa moja jioni kwa udhamini wa VODACOM na COCA-COLA.

Tags: