Jumamosi , 18th Dec , 2021

Masuala ya uzazi yameonekana kumnogea msanii Malkia Karen baada ya kuweka wazi kutamani kupata watoto wanne pekee kwenye maisha yake.

Picha ya msanii Malkia Karen

Malkia Karen ameshea hilo kwenye 'Insta Story' yake baada ya shabiki kumuuliza kwamba ni watoto wangapi amemuomba mungu amjaalie.

Karen akajibu ni watoto wanne pekee, mpaka sasa msanii huyo ana mtoto mmoja wa kiume anayeitwa Celeb.

Pia amemtaja Shetta kuwa ndio msanii wa kwanza kumtembelea baada ya kujifungua.