Mallya afunguka kuhusu Mama Mchungaji na Sheikh

Alhamisi , 6th Mei , 2021

Wahenga walisema mapenzi majani huota popote na hayachagui nchi, rangi, kabila na dini lakini mshauri wa masuala ya mahusiano Rosemary Mallya amesema usiingie kwenye ndoa kama mmoja wa wazazi wenu ni Mchungaji au Sheikh.

Mshauri wa mahusiano Rosemary Mallya

Akizungumzia suala hilo kwenye mada ya dini ina nafasi gani kwenye mahusiano kupitia show ya DADAZ Rosemary Mallya ameeleza kuwa "Kuhusu ndoa kwenye dini inaweza ikawa kikwazo na inaweza isiwe kikwazo kama huelewi nini unataka, kwa sababu kuna watu wameona kwa dini moja lakini bado hawana imani, cha kwanza unatakiwa ujue dini yako inasemaje kabla ya kuingia kwenye ndoa"

"Usiingie kwenye ndoa kwa sababu ya dini, ipende dini kwanza kuliko ndoa hata mkiachana utaendelea kuipenda dini yako, dini isiwe chanzo cha wewe kupata ndoa kwa sababu utakuwa unampenda mume au mkeo na maana dini hutaitumikia vizuri" Rosemary Mallya- Mshauri wa mahusiano

"Ukishajua mama yako ni Mchungaji halafu baba yake ni Sheikh msiingie kwenye mahusiano na mtu wa dini tofauti na hizo, utahitaji ushauri na baraka kutoka kwa wazazi sasa utakapoingia kwenye hiyo ndoa na wazazi wameikataa hautaweza kushaurika"

Interview nzima bonyeza hapa kutazama.