Jumanne , 29th Jul , 2014

Msanii mkongwe wa maigizo kutoka nchini Kenya, Mama Kayai ameweka hisia zake wazi kuwa, binafsi hakuipenda nafasi iliyochezwa na mwigizaji nyota wa kimataifa Lupita Nyong'o, katika filamu maarufu ya "12 Years a Slave".

msanii wa maigizo wa Kenya Mama Kayai

Mama Kayai amesema kuwa hii ni kutokana na sababu za kimaadili, huku akisema kuwa filamu ambazo zinatengenezwa nchini Kenya zinakuwa na ubora mkubwa kuliko zile zinazofanywa huko Marekani.

Msanii huyu amejipatia umarufu mkubwa kupitia vichekesho maarufu vya Vitimbi, sambamba na mumewe wa kimaigizo ambaye anatambulika na mashabiki wake kwa jina Mzee Ojwang.