Jumatano , 13th Apr , 2022

Mapacha watatu Cate, Eve na Mary wamefunguka kutaka kuolewa na mwanaume mmoja baada ya kila mmoja wao kudai wanampenda mwanaume huyo.

Picha ya mapacha watatu na mpenzi wao mmoja

Wadada hao wamesema kuwa kwenye mahusiano na mpenzi mmoja haikuwa jambo gumu kwasababu wao ni ndugu wa karibu sana na wamekuwa wakigawana kila kitu tangu utotoni mwao.

Kwa mujibu wa Cate anasema yeye ndio alikuwa wakwanza kukutana na mwanaume huyo kisha wenzake wakaanza kumpenda na wanatarajia kuolewa hivi karibuni.

Wadada hao hukutana na mpenzi wao kwa siku binafsi kuanzia Jumatatu, Jumanne na Jumatano pia Ijumaa hukutana pamoja kwa ajili ya chakula cha jioni.