Ijumaa , 22nd Jan , 2016

Mwanamuziki nyota wa muziki wa Pop nchini Marekani, Mariah Carey, na bilionea raia wa Australia James Packer wamefunga uchumba na wanampango wa kuoana.

Wawili hao walibainisha penzi lao hilo mbele ya umma mwezi Juni mwaka jana baada ya kuonekana wakiwa pamoja kwenye mapumziko ufukweni nchini Italia.

Packer, mwenye miaka 47 ni tajiri wa wanne kwa utajiri Australia kwa mujibu wa jarida la Forbes, akiwa na utajiri wa dola bilioni 3.1.

Mwanamuziki Mariah Carey, miaka 45 aliyeachia albamu yake ya kwanza 1990 na ni mingoni mwa wasanii wakubwa waliouza mauzo mengi ya kazi zao wa muda mrefu.