
Sugu amesema hayo alipozungumza na ENews ya EATV wakati wa kuaga mwili wa marehemu kwa ajili ya kwenda kuzikwa jijini Tanga.
Mbunge huyo amesema kuwa msanii huyo alikuwa anajituma sana na ilipofika mahali akaona mziki kwake haumlipi akaamua kujiunga katika kazi ya ufundi wa magari jambo ambalo ni jema na mfano kwa wasanii wengine.
Wakati huo huo wasanii wengine kama Keisha,Bwanamisosi,na Daz Baba waliojitokeza wakati wa kuaga mwili wa marehemu nao wameelezea wasifu wa marehemu kwamba alikuwa mtu anaeshirikiana na wasanii wengine na jamii kwa ujumla na mchago wake utakumbukwa katika tasnia ya sanaa ya muziki.
Marehemu John Woka alifariki dunia katika hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kupata jeraha kwenye paji la uso wakati akirekebisha ac ya gari lake.