Ijumaa , 11th Jul , 2014

Mwanafunzi wa kike aliyeripotiwa kuwa ametoweka kwa wiki mbili nchini Uganda amekutwa kwa mwanamuziki Michael Mukwaaya aka Mickie Wine ambaye ni mdogo wa Bobi Wine.

Msanii wa nchini Uganda Mickie Wine

Mama wa mwanafunzi huyo anayekaa Kayunga, amesema ana watoto 14, ambapo binti yake huyo anakaa na mjomba wake huko Kira.

Wazazi wa mwanafunzi huyo walichanganyikiwa baada ya kupata taarifa kuwa hakuwepo shuleni kwa wiki mbili na kufanya polisi kuanzisha msako.

Rafiki yake wa kike aliwaarifu polisi kuwa mwanafunzi huyo amekuwa akionekana kwa mwanamuziki Mickie Wine ambaye anakaa eneo la Magere.

Msanii wa muziki, Mickie Wine, Uganda