''Mimi bado chipukizi'' - Quick Rocka

Alhamisi , 5th Sep , 2019

Imekuwa ni muda sana tangu Rapa Quick Rocka aachie ngoma ambapo Falling ndiyo ilikuwa ngoma ya mwisho kutoka kwake, aliyoiachia rasmi tarehe 26 Septemba mwaka 2018 katika mtandao wa YouTube.

Quick Rocka

Akizungumza na EATV & EA Radio Digital Quick Rocka ameahidi ujio mpya kimuziki ndani ya mwezi wa tisa mwaka huu sababu wamemaliza kushuti tamthiliya ya Kapuni ambayo nae alikuwa mshiriki.

"Tangu mwaka huu uanze sijaachia kazi yoyote sababu nilikuwa bize kurekodi upande wa filamu ambayo naimani watu wameona nilichokifanya huko lakini kwa sasa tumeacha kurekodi hivyo watu wajipange kunipokea tena," alizungumza.

Kuhusu mipango yake upande wa filamu kama kufanya kolabo na waigizaji wengine ambao wapo kwenye tasnia hiyo ndani na nje ya nchi alisema mpango huo upo na kama itatokea atafurahi kwa sababu itazidi kumjenga zaidi.

"Mimi ni msanii mchanga sana wa maigizo bado chipukizi nahitaji kufanya kazi na watu ambao wamenitangulia pia nahitaji kushikwa nao mkono hivyo nitafurahi kama nikipata nafasi hiyo," aliongeza.

Kuhusu kuendelea kusimamia kazi mbalimbali za wasanii Quick anasema kwa sasa anachofanya ni kusapoti tu lakini kama ataamua kufanya hivyo basi atasema.