''Mkisikia nimeachika msishangae'' - Billnas

Alhamisi , 5th Sep , 2019

Billnass amesema muda wowote kuanzia sasa anaweza kuachika na mpenzi wake mpya kutokana na kusambaa kwa picha na video zikionyesha akiwa amerudiana na Nandy katika mitandao ya kijamii.

Nandy na Billnas

Billnass amesema hayo kwenye mahojiano na EATV & EA Radio Digital baada ya kuulizwa kama inamuathiri vipi watu wanaposema amerudiana tena na Nandy.

"Inaniathiri pakubwa kwa sababu mahusiano yangu yapo kwenye changamoto kubwa sana au siku yoyote mkisikia nimeachika msishangae, sisi hatujiachii na hatuko karibu kama ambavyo watu wengine wanaona kwa sababu tangu nimeachia wimbo wa Bugana sijaonana tena na Nandy mpaka leo", ameeleza.

Billnass ameendelea kusema picha na video ambazo wanapost katika mitandao ya kijamii ni za muda walipiga wakati wapo 'Location' wana-shoot video ya Bugana na hataki watu waamini kama wana ukaribu huo.

Wawali hao wamekuwa wanazungumziwa sana na watu katika mitandao ya kijamii kutokana na ukaribu wao unaoonesha kama wamerudiana. Video ya wimbo wao inafanya vizuri tangu itoke ikiwa na siku 5 na imepata watazamaji 736,453.