Jumanne , 21st Apr , 2026

Aliyekuwa msanii wa kundi la P Square Mr P ametangaza kubadili tarehe ya siku yake ya kuzaliwa kutoka Novemba 18 ambayo ndio siku amezaliwa na pacha wake Rude Boy hadi kuwa Tarehe 30 Novemba

Mr P ameeleza kuwa sio tu kubadilisha tu tarehe hata zawadi wala pongezi zozote zitakazokuja siku ya tarehe 18 hatazipokea kutoka kwa mtu yoyote yule.

Uamuzi huu unaaminika ni kutokana na ugomvi uliyopo kati yake na pacha wake ambao umedumu kwa muda mrefu sasa.