Jumapili , 17th Jan , 2016

Nyota wa mashairi ambaye pia ni msanii wa muziki nchini Mrisho Mpoto amesema kuwa amepata presha kutoka kwa mashabiki na watu mbalimbali kuhusiana na ukimya wake wa kuchelewa kutoa kazi na kuonekana kupotea katika sekta hiyo ya muziki.

Nyota wa mashairi ambaye pia ni msanii wa muziki nchini Mrisho Mpoto

Mrisho ameongea na enewz kuwa ameamua kuingia na kukesha studio hapo jana usiku akifanya kazi na wasanii nyota Banana Zorro na mwanadada frida ambao wapo mbioni kutoa nyimbo yao mpya inayoitwa 'Sizonje'

Mrisho aongea zaidi kuhusiana na kazi hiyo mpya ambayo inafanyiwa makeke na mtayarishaji mkali Allan Mapigo na pia kuhusiana na tuzo maarufu za muziki za Kora ambazo amekuwa ni miongoni mwa wasanii nchini waliochaguliwa kuwania katika tuzo hizo kubwa.