Msanii alalamika kutokumbukwa na Alikiba

Jumamosi , 1st Jun , 2019

Msanii wa Bongofleva Spince Seseme, amesema msanii mwenzake ambaye wamewahi kufanyakazi huko nyuma Alikiba hamkumbuki na mara nyingi amekuwa akimtupa kila anapomhitaji.

Alikiba

Akiongea kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Seseme ameweka wazi kuwa ameshamfuata mara nyingi Alikiba ili amsaidie hata kufanya kazi kwenye Label yake ya Kings Music lakini amekuwa hamsikilizi.

''Nishaenda sana kwa Alikiba lakini hanikumbuki ila kuna kupindi aliniomba msamaha mara tatu ila hata anapofanya show zake za mwisho wa mwaka hata hanialiki nimeamua tu abaki mshkaji kama kazi imeshindika'', alifunguka Seseme.

Seseme alishirikiana na Alikiba kwenye ngoma inayoitwa Ayaya ambayo ilifanya vizuri sana mwaka 2012. Ngoma hiyo ilimtambulisha vizuri Seseme na mashabiki wakaamini atafanya poa lakini baadaye akapotea.

Zaidi mtazame hapa.