Msanii wa filamu Wastara Juma aomba msaada

Jumatatu , 3rd Mei , 2021

Msanii wa filamu Wastara Juma ameomba msaada kwa watu wenye uwezo wa kumsaidia kwenye jukumu la kuwapa mahitaji muhimu watoto yatima 53 ambao anawasaidia nyumbani kwake kwa nguvu zake binafsi.

Msanii wa filamu Wastara Juma

Wastara ameomba msaada huo kwenye uzinduzi wa Kampeni ya Mama la Mama ya East Africa TV ambayo ilizinduliwa rasmi siku ya Jumamosi Mei 1,2020 pale Samaki Samaki Mlimani City Dar es Salaam.

"Mimi nawahudumia watoto yatima 53 nyumbani ,nahitaji sana ya watu wenye moyo ili waweze kunisaidia, Mama yeyote asijifu kama analea watoto peke yake kwa sababu kuna mahali kuna sauti ya baba inatakiwa isikike kwenye kulea mtoto" amesema Wastara Juma

Katika uzinduzi huo kulihudhuriwa na baadhi ya mastaa kama Rosa Ree na mama yake, Wastara Juma, Stara Thomas, Mwasiti na Isha Mashauzi.