Jumatatu , 18th Mei , 2020

Kamera man na msanii wa tamthilia ya Wagonga ulimbo na Dakika 90 inayoruka East Africa TV kila siku ya Jumamosi na Jumapili kuanzia 12:00 jioni, John Paul "Nyandu Boy" amefariki dunia kwa ajali ya gari siku ya jana Mei 18,2020

Picha ya marehemu John Paul "Nyandu Boy"

Akitoa taarifa kuhusu chanzo cha kifo chake, ratiba ya mazishi na msiba ulipo msemaji wa familia aitwaye Noster amesema

"Chanzo cha kifo chake ilikuwa ni ajali ya gari iliyotokea saa 12 jioni wakati anatoka beach, gari ilimshinda dereva ikaacha barabara na ikaenda kupiga miti, yeye alitaka kuruka ila miti ya pembeni ikapiga kichwani mwake, msiba upo nyumbani kwao Tegeta Dar Es Salaam na ratiba ya mazishi itakuja muda mfupi maana kuna ndugu zake walikuwa mbali na tunawasubiria" ameeleza Noster 

Kupitia tamthilia ya Wagonga ulimbo marehemu alikuwa ni kamera man ambaye ameshiriki ku-shoot tamthilia hiyo mwanzo mwisho,  na kwenye tamthilia ya Dakika 90 alikuwa ni mshiriki ambaye alitumia jina la Nyandu Boy.