Chambuso ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kutokea maneno katika siku za hivi karibuni kwa baadhi ya watu wakidai kuwa kasi ya Aslay kwenye utoaji nyimbo imepungua huku wengine wakidiriki kusema kwamba hata kipaji chake kimeshuka kutokana na kutoa nyimbo ambazo haziwakongi nyoyo kwa upande wao.
"Tunachokifanya sio kibaya ni kizuri kwa sababu sio kila nyimbo ya Aslay utaipenda nyingine utaiona kawaida, tumekupa ngoma mbili chagua moja utakayoona wewe inakufaa. Kwa hiyo mtu akiona kasi ya Aslay imepungua au kutaka na kumfananisha na mtu fulani atakosea, kwa sababu Aslay anafanya muziki wake yeye kama yeye na hataki kushindanishwa na yeyote na wala hafanyi kwa kutaka sifa kwa watu", amesema Chambuso.
Mtazame hapa chini Chambuso akifunguza zaidi kuhusiana na msanii wake Aslay...

