Jumamosi , 25th Oct , 2014

Baada ya kutoka kwa Remx ya ngoma ya Tupogo ya msanii Ommy Dimpoz meneja wa msanii huyu, Mubenga ameweka wazi kuwa kazi hii imekuja sambamba na mpango wa kuwapatia mashabiki Video ya Tupogo baada ya kushindikana kufanyika kwa Tupogo toleo la kwanza.

Ommy Dimpoz na Mubenga

Mubenga amesema kuwa, kwa wale mashabiki ambao kwa muda sasa wamekuwa wakiuliza juu ya video ya Tupogo, mpango unaendelea sasa kufanya kazi hii kupitia remix ya kazi hii ambayo imeanza kupokelewa vizuri.