Ijumaa , 5th Dec , 2025

Muigizaji Mkongwe na Producer Cary-Hiroyuki Tagawa amefariki dunia jana Disemba 4, akiwa na miaka 75 Santa Barbara, California Marekani.

Picha ya aliyekuwa muigizaji Tagawa

Tagawa amefariki mbele ya familia yake baada ya kuugua kwa muda mrefu ugonjwa wa kiharusi 'Stroke' na taarifa hizo zimedhibitishwa na meneja wake Margie Weiner.

Baadhi ya movie ambazo ameigiza Tagawa ni Mortal Kombat, Bridge of Dragons, Showdown in Little Tokyo, Rising Sun, Big Trouble in Little China, American Me, Ghost, White Tiger, Dangerous.