Jumatatu , 3rd Nov , 2014

Rapa Mwana FA ambaye kwa upande wake kimuziki, Kurap ni sehemu pekee ambayo amejikita kufanya katika muziki wake, amesema kuwa hawezi hata kidogo kujaribu kuimba hata kama ni kipande kidogo.

msanii wa muziki wa bongo fleva Mwana FA

Mwana FA ametoa maoni haya alipokuwa akijadili nafasi ya muziki wa Hip Hop na ule wa kuimba, ambapo amesema kuwa kwa nafasi yake ni rap, kuimba anawaachia waimbaji, na hata ngoma yake ikihitaji sehemu ya kuimba atatafuta mwimbaji wakufanya hivyo.