Jumanne , 3rd Sep , 2019

Mkongwe wa HipHop Bongo, Mwana Fa, ameeleza kuhusu kutaka kufungua darasa la kufundisha watu maisha, ushauri na jinsi watu wanavyotakiwa kuishi kwenye maisha ya sasa na ya baadaye.

Mwana Fa

Mwana Fa ameimbia hayo EATV & EA Radio Digital baada ya kuulizwa kama anaweza kufungua darasa kuhusu kuwafunza watu maisha.

"Siamini kama unaweza kujifunza maisha moja kwa moja kwa kusikiliza maneno ya mtu, naamini kuwa maisha yetu kila siku yanatakiwa yawe darasa hivi vitu vingine vidogovidogo ziwe kama mada za kujifunza kila siku".

Aidha Mwana Fa ameendelea kusema anataka siku akiondoka akumbukwe kama mwalimu na watu waweze kukumbuka vitu alivyokuwa anavisema ili kuvitumia katika maisha yao ya kila siku.

Pia amesema tayari baadhi ya watu wameshaanza kutumia maneno yake yanayotoka kwenye nyimbo zake, kwa kuandika kwenye magari na wengine wakipost katika mitandaoni ya kijamii.

Hata hivyo amesema yeye ndiyo muandishi bora  kwa upande wa wasanii kutokana na kile anachokiandika kwenye ngoma zake na huwa anasikiliza nyimbo za watu wengine anaona bado hakuna wa kumfikia.