
Kulia ni Mwana Fa Mbunge wa Muheza Tanga, kushoto ni Babu Tale Mbunge wa Kusini Mashariki Morogoro
Akiwazungumzia baada ya kupata Ubunge kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020 ambapo Mwana Fa amekuwa Mbunge wa Muheza Tanga, na Babu Tale ni Mbunge wa Kusini Mashariki Morogoro, mtangazaji Dullah Planet amesema
"Ni ushindi kwenye tasnia yetu ya muziki na sanaa kwa ujumla kwa sababu ilikuwa inaonekana sehemu ya kihuni na miyayusho lakini tumeweza kutoa nafasi ya kutoa watu kuwakilisha Bungeni"
"Ni heshima kubwa hongera kwao natumaini wataenda kutekeleza waliyoyaahidi na wananchi wapo tayari kuwaona wakifanya kazi kazi, na sisi tunawaambia wasitutie aibu kwa wananchi kwa sababu wanatoka kwenye upande ambao sisi tupo, tunawategemea kwenye makubwa" ameongeza Dullah Planet
Zaidi tazama hapa chini kwenye video