Ijumaa , 28th Nov , 2014

Kutokana na wasanii na wadau wakubwa wa burudani kuwa na muamko mdogo katika kuzungumza vitu vya msingi vinavyoihusu nchi hususan katika mitandao, rapa MwanaFA amesema kuwa, tatizo hili mara nyingi linasababishwa na uelewa wao mdogo.

msanii wa bongofleva Mwana FA

Rapa huyu amesema kuwa, wakati mwingine kwa mtu ambaye anafanyakazi ya sanaa, wanakuwa wanajiweka mbali na kuzungumza mambo haya kwa kudhani kufanya hivyo kunawaingiza katika mambo ya kisiasa na saa nyingine kuathiri hata mashabiki zao.