Jumamosi , 20th Feb , 2016

Msanii Godfrey Tumaini maarufu kwa jina la Dudu baya, amefunguka juu ya wimbo ambao ulimpa umaaru

Msanii Godfrey Tumaini maarufu kwa jina la Dudu baya, amefunguka juu ya wimbo ambao ulimpa umaarufu wa mwanangu huna nidhamu, na kusema wimbo huo lilikuwa dongo la Master Jay.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Dudu baya alisema aliuandika wimbo huo baada ya kuchukizwa na kitendo cha Master Jay kumtupia pesa yake aliyompa ya kurekodi, baada ya kumjia juu kwa nini hawajerekodi kwa muda kama walivyokubaliana.

“Unajua kipindi hiko mi nilikuwa nakaa Tegeta, na Master jay alikuwa anakaa kwa baba yake, sasa kila Jumamosi ndio alisema njoo urekodi, kipindi hiko na kina Mr. II (Sugu), sasa siku nyingine unakuta dingi kashampa kazi nyingine anafanya, so anakuwa hana muda, siku moja nikamwambia vipi unazingua ujue! Akatutupia hela zetu chini, si ndo tukaenda tukarekodi kwa Minje na ngoma ikawa hiti”, alisema Dudu baya.

Pamoja na hayo Dudu baya amesema ila Master Jay ndio alikuwa producer wake wa kwanza kumpa hela, na alimpa shilingi elfu kumi ambayo kwa kipindi hiko ilikuwa kubwa.

Akiongelea kuhusu msanii ambaye alikuwa chini yake Dogo Hamidu kwa sasa 'Nyandu Toz', Dudu baya amesema anajivunia mafanikio ya msanii huyo, kwani kwake ni kama mtoto wake kwani mama yake alipofariki alimwacha mikononi mwake.

“Unajua hata mama yake Nyandu alivyofariki aliniambia nakuachia mwanangu, nilelee mtoto wangu, na Nyandu hakuwahi kumjua baba yake, so nikawa namlea Nyandu kama mwanangu, nikamwambia dogo sikupeleki studio mpaka usome kwanza. Ndio akaenda shule, ila kwa sasa najivunia mafanikio yake kwani ni sawa na mtoto wangu mwenyewe”, alisema Dudu Baya.

Kuhusu kipigo alichowahi kumpa Nyandu Toz baada ya kuacha chenji ya sh. 300 dukani, Dudu baya alisema alimpiga ili kumfundisha juu ya matumizi ya hela, na si vinginevyo kama watu wanavyofikiria.