Jumatatu , 24th Oct , 2016

Msanii wa muziki wa Bongo Fleva ambaye kwa sasa anafanya vizuri wa wimbo wake wa 'Rarua' Malaika amefunguka na kusema kuwa hakuna mwanaume lijali na mwanaume aliyekamilika ambaye anaweza kuishi kwenye nyumba ya mwanamke.

Malaika

 

Malaika alisema hayo kupitia kipindi cha ujenzi kinachorushwa na EATV alipokuwa akionesha hatua iliyofikia nyumba yake hiyo na kudai kuwa haamini kama kuna mwanaume atakuwa tayari kuja kukaa kwenye nyumba ambayo yeye amejenga kwa jasho lake, Malaika anadai nyumba hiyo ameweza kuijenga kwa pesa za muziki na dili nyingine mbalimbali hivyo alianza mdogo mdogo mpaka sasa anakaribia kuhamia.

"Sidhani kama kuna mwanaume lijali, mwaume kamili ambaye anaweza kuishi kwenye nyumba ya mwanaume, au nyumba aliyojenga mwanamke, dunia ya leo ukiona mwanamke ana gari zuri, nyumba nzuri lazima hapo mwanaume ujipange. Hivyo sidhani kama mwanaume atatoka mwanaume huko aliko na kuja kuishi kwangu" alisema Malaika