Alhamisi , 28th Mei , 2015

Kufuatia uvumi kuhusiana na kufika mwisho kwa kipindi bora na mahiri kwa upande wa sekta ya burudani Tanzania cha Planet Bongo, mtangazaji wa kipindi hicho, Dulla aka Mjukuu wa Ambua aongea na eNewz kuthibitisha taarifa hizo.

mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo cha EATV Dulla aka Mjuku wa Ambua

Kwa mujibu wa mjukuu habari hizi zimeendelea kuwa gumzo mtandaoni huku mashabiki na wadau wengi wa kipindi hicho wakijiuliza nini haswa sababu ya kipindi hicho kufikia tamati baada ya Dullah kukiendesha kwa takribani miaka saba hadi sasa.

Kuhusiana na tetesi hizo, huyu hapa Dullah anaeleza kwa undani zaidi.