Jumatatu , 4th Jan , 2016

Mwanamuziki wa Hip Hop kutoka Mombasa nchini Kenya Kaa la Moto amemshirikiana Mkongwe wa mtindo wa Bango nchini humo Mzee Ngala na kusema amefanya hivyo ili watu wajue mziki wa hip hop ni wa rika zote.

Mwanamuziki wa Hip Hop kutoka Mombasa nchini Kenya Kaa la Moto

Akiongea na eNewz Kaa la Moto ambae ameachia wimbo huo alioupa jina la 'Nisikilize Mwanangu' amesema ameamua kufanya muziki huo kiafrika zaidi kuweza kuufanya muziki mzuri uendelee kuishi.

Kaa la Moto ambae ametoa nyimbo mfululizo amesema sababu kubwa ni inspiration kutoka kwa mashabiki wake ambao wanapenda kumsikia mara kwa mara akiachia ngoma kali na kutaka ladha tofauti.