Jumanne , 13th Nov , 2018

Msanii wa Bongofleva Mwasiti amempongeza Nandy kwa kuzindua Album yake wikiendi iliyopita na kumshauri kwamba asije akalewa umaarufu na kupasuka kichwa kwani 'atakufa' na kupotea kabisa kwenye sanaa.

Mwasiti kushoto na Nandy kulia.

Akiongea kupitia eNEWZ Mwasiti amesema msanii kama ana kipaji kukuwa na kupata umaarufu ni rahisi sana ila kama ukilewa umaarufu huo ni lazima upotee kwenye sanaa kwa muda mfupi sana kwa kuwa muziki unahitaji heshima na nidhamu ya hali ya jiji ili kuweza kuishi na kufanya vizuri katika sanaa.

"Mimi ninamfahamu Nandy vizuri binti mdogo mwenye malengo makubwa, lakini pia ananidhamu  na ni mtafutaji, anakipaji na anajua kwamba anaweza hivyo kama akilewa sifa na kichwa kuwa kikubwa atapotea haraka sana kwenye sanaa maana hii kazi yetu ni lazima uipende na uiheshimu  ili kuweza kudumu katika sanaa kama sisi tulivyofanya"aliongea Mwasiti 

Pia Mwasiti alimalizia kwa kutoa wito kwa wasanii wenzake ambao wana mipango ya kutoa albam zao hivi karibuni kwamba wakitoa albam wajipange kuzisapoti na kuzitangaza kwani kutoa album sio kitu rahisi tu sapoti inahitajika katika kuisambaza kama walivyofanya Vanessa na Barnaba katika kutangaza albam zao.