Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Nataka mume, sipendi dhambi - Khadija Kopa

Jumatano , 21st Mar , 2018

Malkia wa Mipasho nchini Tanzania asiyekuwa na mshindani, Khadija Kopa ametangaza rasmi kuhitaji mume wa kumuoa ili aweze kuishi naye huku akiweka vigezo vyake kuwa hataki aliyechini ya miaka 40 kwa madai hawezi kufundisha tution.

Khadija Kopa ametoa kauli hiyo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa mubashara kupitia kurasa za EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa 8:00 mchana hadi 10:00 alasiri.

"Sijaolewa ila sitaki kusomesha tuition, nataka mwanaume aliyekuwa na umri mkubwa kuanzia 40 kwenda juu, mwenye mapenzi ya dhati na huba, mwenye kujali na kujua ninataka nini, atakayeweza kuijali familia yangu pamoja na watoto wangu, awe mnene kidogo na sio mwembamba, awe na rangi yeyote na kabila lolote lile kwasababu mimi sina ubaguzi katika vitu hivyo", amesema Khadija Kopa.

Pamoja na hayo, Khadija Kopa ameendelea kwa kusema "napenda mwanaume mfanyakazi maana kupata pesa ni majaliwa ila asiwe mwanaume wa kulala nyumbani akanitegemea mimi nikafanye kazi ili yeye aje kula maana maisha ni kusaidia nasio kuegemea upande mmoja tena wa mwanamke".

Aidha, Khadija Kopa amesema sababu kubwa iliyompelekea mpaka sasa kutoolewa ndoa nyingine baada ya aliyekuwa mume wake kufariki ni kutokana na kuwa na wasiwasi na wanaume wa sasa.

"Nina wasiwasi kwa mwanaume atakayekuja kunioa kwa sasa, maana najiuliza mengi je atakuwa na huba kama marehemu mume wangu ndio maana mpaka sasa sijaolewa kwa kuwa nafikiria sana. Mume wangu aliyefariki alikuwa ni mwenye huba, mwenye kunijali, nimekaa naye miaka yote sijawahi kugombana naye, nilikuwa natamani kumuona akinuna ananuna vipi, alikuwa na vigezo vyote", amesisitiza Khadija Kopa.

Mtazame hapa chini Khadija Kopa akifunguka mengine zaidi.

 

HABARI ZAIDI

Muonekano wa Eneo la Somanga baada ya Mawasiliano kati ya Lindi na Dar es Salaam kurejeshwa.

Mawasiliano yarejeshwa barabara ya Dar - Lindi

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga

Kituo cha kupoza umeme kujengwa Tunduma

Mkuu wa Usalama Barabarani mkoa wa Songwe Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Charles Bukombe, akizungumza na abiria

"Fungeni mikanda muda wapo safarini" - SSP

Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi

"Ndege ijayo ipewe jina la Mwl Nyerere" - Profesa

Baadhi ya Wanachi wa Kata ya Msowero, wakiwa Katika Mkutano wa Hadhara na Mkuu wa Wilaya

Mwenyekiti atiwa mbaroni kwa kuuza mlima, Msowero

Sehemu iliyokumbwa na Mafuriko Kusini mwa Brazil

Wanaokufa kutokana na mafuriko waongezeka Brazil