Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Nay wa Mitego amkana JPM, BASATA wampandia hewani

Jumanne , 9th Oct , 2018

Msanii wa muziki wa Bongo fleva Emmanuel Elibariki maarufu kama 'Nay wa Mitego',amekanusha uvumi kuhusiana na kauli yake ya 'Zote kwa John' iliyopo katika wimbo wake mpya wa "ALISEMA" kuwa alimlenga Rais John Pombe Magufuli.

Akipiga stori na www.eatv.tv Nay amesema ametumia tafsida ya John kumuonesha kiongozi anayefanya mambo mazuri kwa jamii yake na pia anaweza kulaumiwa endapo atakiuka maadili katika kuwatumikia wananchi wake.

"Kwa sasa John ndio anaye laumiwa,ukizungumza mazuri ya John basi zungumza na mabaya yake pia kama binadamu anavyotenda mema na mabaya, hawezi fanya mazuri peke yake, sitaki kusema John gani, mimi ni msanii, natumia sanaa yangu kuweka mafumbo ili kufikisha ujumbe kwa hadhira, ukweli naujua mimi ambaye nimemuongelea",  amesema Nay wa Mitego.

"Huu ni wimbo ambao una tafsiri nyingi sana, unahitaji utulize akili, unahitaji uwe na mawazo mapana ili uelewe,unahitaji ujiulize je ni wangu? au unanihusu mimi?, nafkiri nimejaribu kutumia tafsida na akili nyingi ili kila mtu anaye usikiliza aweze kutoka na tafsiri yake", ameongeza Nay.

Pia Nay wa Mitego amesema wimbo huo umemletea sifa nyingi baada ya kupokea simu za pongezi kutoka viongozi wengi hapa nchini na simu iliyo mshtua ni kutoka kwa kiongozi BASATA.

"Tangu nilipoachia wimbo huo nimepokea simu nyingi kutoka kwa viongozi wengi na wengine kutoka serikalini wakinipongeza, lakini simu iliyonishtua ni kutoka kwa kiongozi wa BASATA akaniambia sizungumzii BASATA ila nimekupigia simu kukupa pongezi ya wimbo wako mimi kama mimi binafsi nimeupenda, nilifurahi sana kusikia hilo, ila mpaka sasa sijapokea simu kutoka kwao".

HABARI ZAIDI

Mbunge wa Kilosa Profesa Palamagamba Kabudi

"Ndege ijayo ipewe jina la Mwl Nyerere" - Profesa

Baadhi ya Wanachi wa Kata ya Msowero, wakiwa Katika Mkutano wa Hadhara na Mkuu wa Wilaya

Mwenyekiti atiwa mbaroni kwa kuuza mlima, Msowero

Sehemu iliyokumbwa na Mafuriko Kusini mwa Brazil

Wanaokufa kutokana na mafuriko waongezeka Brazil

Baadhi ya Wabunge Wakichangia Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Uchukuzi

Serikali yashauriwa kuwa bunifu sekta ya usafiri

Baadhi ya Wananchi Wakishudia Ajali Iliyomgonga Mwendesha Bodaboda

Watatu wanusurika kifo, scania ikimgonga bodaboda

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Deogratius Ndejembi (kulia) pamoja na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama na Mazingira kutoka GGML, Dk Kiva Mvungi (kushoto) wakimpatia vifaa kinga mmoja wa washiriki wa mafunzo kwa madereva bodaboda wa jiji la Arusha.

Bodaboda 200 Jijini Arusha wanolewa na kufundwa