Alhamisi , 15th Dec , 2016

Meneja wa msanii Belle 9 anayefahamika kwa jina la Aza amesema ingawa walikuwa kimya kwa muda mrefu Belle 9 hataachia ngoma mpaka atakapopata followers wapya laki 3 instagram.

Belle 9

 

Akizungumza na Planet Bongo ya East Afrika Radio, meneja Aza amesema huo ndio mtindo mpya waliojiwekea ili kuleta utofauti katika mfumo wa uachiaji wa kazi mpya, ingawa albam tayari ipo katika hatua za mwisho.

“Tulikuwa tunasoma game tukasema haina haja ya kutoa ngoma pap pap, kwanza tuwe tuna ngoma, so far tuna ngoma 22 tunaselect nyimbo 15 kwenye albam ambayo sasa hivi inafanyiwa mastering, from this point kila tukizidisha followers laki 3 from instagram ujue kuna ngoma inakuja, sasa hivi kuna laki nne, ikifika laki 7 kuna ngoma nyingine, ikifika milioni kuna nyingine, follow belle 9”, alisema Meneja Aza.

"Well.... mashabiki kama mnataka kitu kipya kutoka kwa Belle 9, basi mshajua nini cha kufanya, nendeni tu kwenye acount yake na nyinyi mtazawadiwa ngoma mpya" amesema.