Ommy Dimpoz adai hawachukii mastaa wa kike Bongo

Jumatatu , 2nd Dec , 2019

Staa wa BongoFleva Ommy Dimpoz, amefunguka kuwa yeye sio mtu wa kuweka mahusiano yake wazi, pia hana matatizo yoyote na mastaa wa kike Bongo, japokuwa huwa haonekani akiwa nao karibu.

Msanii wa Muziki nchini Tanzania, Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, amesema ana maisha yake ya kawaida na binafsi na kwamba hana chuki na wanawake wa Bongo.

"Nafikiri kuna maisha binafsi na maisha ya kawaida, kuna muda kama msanii unahitaji maisha yako binafsi, halafu mimi sio mtu wa mahusiano yangu kuyaweka wazi, nina upendo wa kutosha na wanawake wote wa Bongo kwa hiyo sina tatizo nao wala siwachukii" amesema Ommy Dimpoz.

Akizungumzia kuhusu kutoonekana akiwa nao karibu na wanawake mastaa Ommy Dimpoz ameeleza kuwa, "Karibia wote ni marafiki zangu na tunashirikiana kwenye mambo mengi, nafikiri ukaribu sio lazima tuwe nao mitandaoni na mimi sijaweka sana kwenye mitandao, lakini tupo poa na vizuri kabisa" ameongeza.