Jumatano , 27th Aug , 2014

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Mez B amemwachia mikoba kwa sasa mdogo wake anayejulikana kwa jina la One Six anayefanya muziki wa RnB, Soul, Afro Pop na Sweet Reggae.

msanii wa muziki wa bongo One Six

One Six ameiambia enewz kuwa ukimya wa kaka yake Mez B umetokana na kuwa bize mno kwenye mishe zake za utafutaji maisha hivyo ipo siku atarudi ndani ya game, hivyo kwa sasa One Six ametambulisha leo kichupa chake kipya hapa EATV kilichobatizwa jina 'Maya' ikiwa ni project yake mpya iliyofanyika Biorn Records chini ya prodyuza Dash Touches.

Akiwa anafanya kazi zake chini ya menejimenti yake mpya inayosimamia kazi zake chini ya Prince George, One six ameelezea kuwa video hiyo imetengenezwa na kampuni ya After DayLight Films chini ya muongozaji Erick Backamaz.