Jumatano , 10th Nov , 2021

Msanii Otile Brown kutoka 254 nchini Kenya, amedai kuchukuliwa melody zake za wimbo wa 'baby love' kutumika kwenye wimbo mpya wa Mbosso na Zuchu uitwao 'For your love'

Kushoto ni Zuchu na Mbosso kulia ni Otile Brown

Otile Brown ameweka taarifa hiyo kwenye page yake ya Instagram kwa kupost video ya wimbo wa Mbosso na Zuchu kisha akaandika ujumbe ufuatao.

"Punguzeni mazoea basi, hiyo ni melody nzima ya baby love , if you know you know, mna bahati sina utoto na roho mbaya

Video ya wimbo huo wa Mbosso na Zuchu imetoka leo na ina views 92,574 pia ipo trending namba 21 kwenye mtandao wa Youtube.