
Hata hivyo, Diddy ameepuka mashtaka matatu mazito zaidi yaliyokuwa yanamkabili, ikiwemo mashtaka mawili ya ulanguzi wa binadamu kwa ajili ya ngono na shtaka moja la uhalifu wa mtandao (racketeering). Mashtaka hayo yaliyofutwa yalikuwa na uwezekano wa kumuweka jela kwa miongo kadhaa endapo angepatikana na hatia.
Kwa sasa, Diddy anakabiliwa na uwezekano wa kifungo cha hadi miaka 20, kwani kila kosa la kusafirisha watu kwa ajili ya ukahaba linaweza kuadhibiwa kwa hadi miaka 10 gerezani.
Majaji walitoa uamuzi wao baada ya kusikiliza ushahidi kutoka kwa mashahidi wa upande wa mashtaka, wengi wao wakiwa ni watu waliodai kuwa waathirika wa mipango ya muda mrefu ya unyonyaji wa kingono, ambayo kwa mujibu wa mashtaka ilihusisha matumizi ya nguvu, vitisho na mtandao mpana wa watu.
Upande wa utetezi bado haujatoa taarifa rasmi baada ya hukumu hiyo, lakini wakili wake, Marc Agnifilo, hapo awali aliieleza mahakama kuwa mteja wake hakuwahi kuhusika katika shughuli yoyote ya kihalifu na alikuwa akilengwa kwa sababu ya umaarufu wake.
Tarehe ya kusomwa kwa adhabu rasmi bado haijatangazwa, lakini wachambuzi wa masuala ya sheria wanasema kesi hii inaweza kuwa na athari kubwa kwa sifa ya rapa huyo pamoja na tasnia ya muziki ya Marekani kwa ujumla.