Ijumaa , 15th Jan , 2016

Pauline Zongo mwanamuziki ambaye amerudi hivi sasa kuonesha uwezo wake katika muziki amesema kuwa huu utakuwa ni mwaka wake mpya baada ya kuwa bize na maswala ya kifamilia ambazo pia zimechangia kuwa kimya nje ya muziki.

mwanamuziki Pauline Zongo wa nchini Tanzania

Nyota huyo hivi sasa amejiwekeza zaidi kupiga muziki wake kama bendi katika mahoteli mbalimbali maarufu jijini Dar es salaam, ameiambia eNewz kuwa anakamilisha taratibu zake za kulizindua kundi lake jipya liitwalo 'Too Big' na pia albam yake mpya itakayokuwa zawadi ya kushtukiza kwa mashabiki wake.